Jina, sarafu na nembo
- 1. Kwenye menyu fungua Mipangilio > Mipangilio ya Biashara. Utafungukia kichupo cha Biashara.
- 2. Badilisha Jina la Biashara ukihitaji.
- 3. Kagua Sarafu na Uwekaji wa Alama ya Sarafu.
- 4. Kagua Saa za eneo. Saa zikiwa sahihi, ripoti za kila siku zinakuwa sahihi.
- 5. Kwenye Pakia Nembo chagua picha ya nembo. Nembo ya awali, kama ipo, itabadilishwa.
- 6. Gusa Sasisha Mipangilio chini ya ukurasa.
Maelezo ya risiti
Risiti inachukua maandishi yake kwenye muundo wa ankara, si kwenye mipangilio ya biashara. Hata nembo ya risiti inawekwa hapa, kwa hiyo iweke hata kama umeshapakia nembo hapo juu.
- 1. Fungua Mipangilio > Mipangilio ya Ankara, kisha kichupo cha Miundo ya Ankara.
- 2. Gusa muundo unaotumika. Muundo unaotumika mara ya kwanza una alama ya Chaguo-msingi.
- 3. Kwenye Nembo ya Ankara chagua picha, kisha weka alama kwenye Onyesha Nembo ya ankara.
- 4. Andika Maandishi ya kichwa na Mstari wa kichwa kidogo 1, kwa mfano jina la mtaa na namba ya simu.
- 5. Kagua Kichwa cha ankara na uweke alama kwenye Onyesha jina la biashara kama unataka lionekane.
- 6. Andika Maandishi ya chini, kwa mfano sera yako ya kurudisha bidhaa.
- 7. Gusa Sasisha.
Namba za ankara
Kwenye Mipangilio ya Ankara, kichupo cha Mifumo ya Ankara, unaweza kuona na kuongeza mfumo wa kuweka namba. Kila mfumo una Kiambishi awali na Aina ya Kuweka Namba. Unachagua mfumo gani utumike kwenye kila tawi, angalia matawi.
Risiti ya DukaPOS ni ya aina gani?
Risiti ya DukaPOS ni risiti ya biashara. DukaPOS si mashine ya EFD na haijaunganishwa na TRA. Biashara yako ikiwa inatakiwa kutoa risiti ya EFD, endelea kutumia mashine yako ya EFD kama kawaida.
Kubadilisha lugha
Lugha inawekwa kwa kila mtumiaji, si kwa biashara nzima. Hivyo mmiliki anaweza kutumia Kiingereza na muuzaji Kiswahili.
- 1. Gusa jina lako juu kulia, kisha Wasifu.
- 2. Kwenye Lugha chagua Swahili - Kiswahili au English.
- 3. Gusa Sasisha chini ya ukurasa.