Ongeza msambazaji
Fungua Anwani > Wasambazaji na uongeze msambazaji. Unaweza pia kumwongeza kwa kitufe cha + kwenye fomu ya manunuzi.
Rekodi manunuzi
Kama menyu ya Manunuzi haionekani, moduli yake imezimwa au huna ruhusa. Mmiliki anaiwasha kwenye Mipangilio ya Biashara, kichupo cha Moduli.
- 1. Fungua Manunuzi > Ongeza Manunuzi.
- 2. Chagua Msambazaji.
- 3. Namba ya Kumbukumbu ukiiacha wazi, itatengenezwa yenyewe.
- 4. Kagua Tarehe ya Manunuzi.
- 5. Kwenye Hali ya Manunuzi chagua Imepokelewa ikiwa mzigo umefika.
- 6. Ukiwa na matawi zaidi ya moja, chagua Eneo la Biashara linalopokea mzigo.
- 7. Kwenye kisanduku cha utafutaji, andika jina au SKU, au skani barcode. Bidhaa itaingia kwenye jedwali.
- 8. Jaza Kiasi cha Manunuzi na Gharama ya Kipimo (Kabla ya Punguzo).
- 9. Kagua Bei ya Kuuza ya Kipimo. Inabadilika hapa tu kama mmiliki amewasha Washa kuhariri bei ya bidhaa kwenye skrini ya manunuzi kwenye Mipangilio ya Biashara, kichupo cha Manunuzi.
Hali ya manunuzi inamaanisha nini?
- Imepokelewa: bidhaa zinaongezeka kwenye stoo na zinaweza kuuzwa.
- Inasubiri na Imeagizwa: manunuzi yanaandikwa, lakini stoo haiongezeki bado.
- Mzigo ukifika baadaye, fungua Orodha ya Manunuzi, gusa Vitendo kwenye manunuzi hayo, kisha Sasisha Hali.
Lipa msambazaji
Chini ya fomu kuna sehemu ya Ongeza malipo. Andika kiasi ulicholipa na njia ya malipo. Kama hujalipa kila kitu, kiasi kilichobaki kinaonekana kwenye Deni la malipo, nacho kinabaki kama deni la msambazaji.
Ukimaliza, gusa Hifadhi. Deni likilipwa baadaye, fungua Orodha ya Manunuzi, gusa Vitendo, kisha Ongeza malipo.
Bidhaa mpya na lebo
Kama bidhaa haipo kwenye mfumo, gusa Ongeza bidhaa mpya kwenye fomu ya manunuzi. Baada ya kuhifadhi, kwenye Orodha ya Manunuzi kitufe cha Lebo kinakuwezesha kuchapisha lebo za mzigo huo.
Tofauti ikionekana kati ya mzigo na rafu, tumia marekebisho ya stoo.