DukaPOS

Jinsi ya kutumia

Jinsi ya kuongeza wafanyakazi, majukumu na ruhusa

Kila mfanyakazi awe na akaunti yake. Hivyo unajua nani aliuza nini, na kila mtu anaona kile tu anachopaswa kuona. Kazi hii inafanywa na mmiliki au mtu mwenye ruhusa ya watumiaji.

Imesasishwa 8 Novemba 2026

Majukumu mawili yaliyopo tayari

Unapojisajili, mfumo unatengeneza majukumu mawili:

  • Admin: anaweza kila kitu. Hili ndilo jukumu la mmiliki.
  • Cashier: anaweza kuuza kwenye POS, kuhariri na kufuta mauzo ya POS, kuona na kufunga rejista, kwenye matawi yote. Ruhusa ya kutoa punguzo haipo mwanzoni.

Rekebisha ruhusa za muuzaji

Kama muuzaji hawezi kuchapisha risiti, fungua jukumu lake na uwashe ruhusa ya Chapisha Ankara. Akaunti za zamani zinaweza kuhitaji hili.

  • 1. Fungua Usimamizi wa Watumiaji > Majukumu.
  • 2. Gusa Hariri kwenye Cashier.
  • 3. Kwenye sehemu ya POS, weka alama kwenye Chapisha Ankara.
  • 4. Ikiwa muuzaji anatakiwa kutoa punguzo, weka pia alama kwenye Hariri punguzo la bidhaa kwenye skrini ya POS.
  • 5. Hifadhi.

Tengeneza jukumu lako

  • 1. Kwenye Majukumu, gusa Ongeza.
  • 2. Andika Jina la Jukumu, kwa mfano Msimamizi wa Tawi.
  • 3. Kwenye Ruhusa, weka alama kwenye anachoweza kufanya. Chagua vyote inatia alama kwa kundi zima.
  • 4. Gusa Hifadhi.

Ongeza mtumiaji

Idadi ya watumiaji inategemea kifurushi chako; ukifikia kikomo mfumo utakuambia.

  • 1. Fungua Usimamizi wa Watumiaji > Watumiaji, gusa Ongeza.
  • 2. Andika Jina la Kwanza na Barua Pepe. Barua pepe ni lazima.
  • 3. Acha alama kwenye Inatumika?.
  • 4. Kwenye Majukumu na Ruhusa, acha alama kwenye Ruhusu kuingia.
  • 5. Jina la mtumiaji ukiliacha wazi litatengenezwa lenyewe. Ni bora ukaliandika.
  • 6. Weka Nywila na Thibitisha Nywila.
  • 7. Chagua Jukumu.
  • 8. Kwenye Fikia maeneo, chagua Maeneo Yote au tawi analofanyia kazi tu.
  • 9. Ukitaka kikomo cha punguzo, jaza Asilimia ya juu ya punguzo la mauzo.
  • 10. Gusa Hifadhi, kisha mpe jina la mtumiaji na nywila.

Mfanyakazi akiacha kazi

Fungua Watumiaji, hariri akaunti yake na uondoe alama kwenye Inatumika?. Hawezi kuingia tena, na kumbukumbu za mauzo yake zinabaki.

Maswali

Maswali ambayo wenye maduka hutuuliza

Muuzaji anaweza kuona faida ya duka?

Jukumu la Cashier halina ruhusa ya ripoti. Ripoti inaonekana tu kama umetoa ruhusa yake kwenye jukumu la mtu huyo.

Kwa nini risiti haitoki kwa muuzaji wangu?

Jukumu lake halina ruhusa ya Chapisha Ankara. Fungua jukumu hilo, weka alama na uhifadhi.

DukaPOS

Fungua duka lako kwenye DukaPOS leo

Fungua akaunti, ongeza bidhaa zako na ufanye mauzo yako ya kwanza leo.