Chapisha lebo za bidhaa
Unahitaji ruhusa ya kuangalia bidhaa. Unaweza pia kufungua ukurasa huu kwa Lebo kwenye Vitendo vya bidhaa, au kwenye Orodha ya Manunuzi kwa mzigo mzima.
- 1. Fungua Bidhaa > Chapisha lebo.
- 2. Kwenye sehemu ya Ongeza bidhaa ili kutengeneza Lebo, andika jina la bidhaa na uichague.
- 3. Jaza Idadi ya lebo kwa kila bidhaa.
- 4. Kwenye Taarifa za kuonyesha kwenye lebo, chagua kama Jina la bidhaa, Bei ya bidhaa au Jina la biashara vionekane.
- 5. Chagua Mpangilio wa msimbo pau unaolingana na karatasi yako.
- 6. Gusa Onyesho la awali na ukague lebo.
- 7. Gusa Chapisha chini ya onyesho, kisha chagua printa yako kwenye dirisha la kivinjari.
Ukubwa wa lebo
Ukubwa na idadi ya lebo kwenye karatasi vinawekwa kwenye Mipangilio > Mipangilio ya msimbo pau. Unahitaji ruhusa ya mipangilio ya barcode. Hapo unaweza kugusa Ongeza mpangilio mpya kwa karatasi yako na kuweka Upana wa karatasi.
Bidhaa ikiwa na barcode iliyochapishwa kiwandani, huhitaji lebo. Skani barcode hiyo kwenye sehemu ya SKU wakati wa kuongeza bidhaa.
Unganisha printa ya risiti
Njia inayotumika mwanzoni ni kuchapisha kupitia kivinjari. Printa ya USB, Bluetooth au ya mtandao inafanya kazi ikiwa imewekwa kwenye kifaa chako. Weka printa kama kawaida ya kifaa, kisha:
- 1. Fungua Mipangilio > Maeneo ya Biashara, gusa Mipangilio kwenye tawi.
- 2. Kwenye Mipangilio ya Risiti, hakikisha Aina ya Printa ya Risiti ni Kuchapisha Kupitia Kivinjari.
- 3. Weka Chapisha ankara kiotomatiki baada ya kumaliza kuwa Ndiyo, ili risiti itoke kila mauzo.
- 4. Gusa Sasisha.
- 5. Fanya mauzo ya majaribio. Dirisha la kuchapisha likifunguka, chagua printa yako. Kwenye kompyuta nyingi unaweza kuweka printa ya risiti kuwa printa ya msingi.
Printa iliyosanidiwa
Pia kuna chaguo la Tumia Printa ya Risiti Iliyosanidiwa na menyu ya Mipangilio > Printa za Risiti. Hii inahitaji programu ya ziada ya kuunganisha printa kwenye kompyuta. Kabla ya kutumia chaguo hili, tupigie 0760550617.
Yaliyomo kwenye risiti, kama nembo na maandishi, yanawekwa kwenye mipangilio ya biashara. Kuchagua vifaa, soma vifaa vya POS. Muuzaji anahitaji ruhusa ya Chapisha Ankara.
Ukihitaji msaada wa printa, piga au tuma WhatsApp 0760550617.