Kuweka maelfu ya bidhaa bila kuziandika moja moja
Ingiza orodha ya bidhaa, bei na stoo ya mwanzo kutoka spredishiti. Bidhaa zenye barcode ya mtengenezaji zinaskaniwa kama zilivyo; kwa bidhaa zisizofungwa na unazofunga mwenyewe, chapisha lebo zenye barcode zako, majina na bei kutoka DukaPOS.
Panga bidhaa kwa aina na chapa ili ripoti, punguzo na hesabu za stoo zifanyike rafu kwa rafu.
Kaunta, makeshia na hesabu ya mwisho wa zamu
Kila keshia anaingia kwa akaunti yake na kufungua rejista yake ya pesa. Mwisho wa zamu anaifunga: taslimu, pesa ya simu na kadi zinahesabiwa kila moja dhidi ya kile DukaPOS ilichotarajia, hivyo upungufu unahusishwa na kaunta moja na zamu moja.
Makeshia wanaona wanachohitaji tu. Kubadilisha bei, punguzo kubwa, kufuta mauzo na ripoti za faida vinabaki kwa mwenye biashara au meneja.
Bidhaa freshi, za kupima na zinazouzika haraka
Nyama, mboga na bidhaa nyingine za kupima zinaweza kuuzwa kwa barcode zinazochapishwa na printa ya lebo ya mzani: DukaPOS inasoma bidhaa na uzito kutoka kwenye barcode. Bidhaa zenye tarehe ya kuisha muda zinaweza kuwa na namba za batch na tarehe, na ripoti inaonyesha zinazokaribia kuisha muda ili zipunguzwe bei mapema.
Kununua kwa usahihi
Weka kiwango cha kuagiza upya kwa kila bidhaa. Orodha ya bidhaa zilizo chini ya kiwango inakuwa oda yako ya manunuzi inayofuata; mzigo ukifika, upokee dhidi ya oda na stoo pamoja na salio la msambazaji vinabadilika pamoja. Ripoti ya mauzo ya bidhaa inaonyesha zinazouzika na zinazokaa rafuni tu.
Endesha punguzo kwa kipindi fulani kwa bidhaa, chapa au aina ulizochagua, na uwazawadie wateja wa kudumu pointi ukitaka.