Nani anaweza na kuna kikomo gani?
Unahitaji ruhusa ya mipangilio ya biashara, kama aliyonayo mmiliki. Idadi ya matawi inategemea kifurushi chako. Ukifikia kikomo, mfumo utakuambia na hautafungua fomu; angalia vifurushi.
Ongeza tawi
- 1. Fungua Mipangilio > Maeneo ya Biashara.
- 2. Gusa Ongeza. Dirisha la Ongeza eneo jipya la biashara litafunguka.
- 3. Andika Jina la tawi.
- 4. Jaza Jiji, Msimbo wa Posta, Mkoa na Nchi. Sehemu hizi ni lazima.
- 5. Alama ya Eneo, Simu ya Mkononi na Barua Pepe si lazima, lakini zinaweza kutumika kwenye risiti.
- 6. Chagua Mfumo wa ankara kwa POS na Mfumo wa ankara kwa mauzo.
- 7. Chagua Muundo wa ankara kwa POS na Muundo wa ankara kwa mauzo.
- 8. Chini kwenye Njia za Malipo, acha alama ya Washa kwenye njia zinazotumika kwenye tawi hili.
- 9. Gusa Hifadhi.
Baada ya kuongeza tawi
Tawi jipya linaanza bila bidhaa wala stoo. Fanya mambo haya matatu:
- 1. Fungua kila bidhaa inayouzwa huko na uongeze tawi hili kwenye Maeneo ya Biashara ya bidhaa, angalia kuongeza bidhaa.
- 2. Leta stoo kwa manunuzi au kwa uhamisho kutoka tawi jingine.
- 3. Mpe muuzaji ruhusa ya tawi hilo kwenye Fikia maeneo, angalia watumiaji na majukumu.
Kubadilisha au kufunga tawi
Kwenye orodha ya Maeneo ya Biashara, kila tawi lina vitufe vyake:
- Hariri: badilisha taarifa za tawi na njia za malipo.
- Mipangilio: chagua muundo wa risiti na namna ya kuchapisha, angalia printa na lebo.
- Zima Eneo: tawi lisilotumika linazimwa badala ya kufutwa. Unaweza kuliwasha tena kwa Wezesha Eneo.
Ukikwama, piga au tuma WhatsApp 0760550617.