Fungua POS
Gusa POS juu ya ukurasa, au fungua Uza > POS. Kama hujafungua rejista, mfumo utakuomba uifungue kwanza.
Weka bidhaa
- 1. Kwenye kisanduku cha mteja, Walk-In Customer ndiye mteja wa kawaida. Kwa mauzo ya mkopo, chagua mteja wake.
- 2. Kwenye kisanduku chenye maandishi Andika jina la bidhaa / SKU / Skani msimbo pau, skani barcode au andika jina.
- 3. Au gusa picha ya bidhaa upande wa kulia. Kwenye simu, gusa Angalia Bidhaa kwanza.
- 4. Badilisha Idadi ikihitajika.
- 5. Jumla ya Kulipa inaonekana chini.
Weka punguzo
Punguzo linaonekana kwa wale wenye ruhusa ya Hariri punguzo la bidhaa kwenye skrini ya POS. Jukumu la Cashier halina ruhusa hii mwanzoni, angalia majukumu.
- 1. Karibu na Punguzo, gusa alama ya kuhariri. Dirisha la Hariri Punguzo litafunguka.
- 2. Chagua Aina ya Punguzo: Kiasi Maalum au Asilimia.
- 3. Andika Kiasi cha Punguzo, kisha Sasisha.
- 4. Kwa punguzo la bidhaa moja au kubadilisha bei yake, gusa jina la bidhaa kwenye jedwali.
Maliza mauzo
Chini ya skrini kuna vitufe vya malipo. Chagua kinachofaa:
- Fedha Taslimu: mteja amelipa kila kitu taslimu. Mauzo yanakamilika hapo hapo.
- Kadi: inafungua maelezo ya malipo ya kadi. Kadi yenyewe inapitia mashine yako ya kadi.
- Malipo Mengi: kwa malipo ya njia zaidi ya moja au pesa kwa simu. Maliza kwa Kamilisha Malipo.
- Mauzo ya Mkopo: mteja atalipa baadaye, angalia madeni.
- Simamisha: weka mauzo pembeni, uendelee na mteja mwingine. Yaangalie tena kwa Angalia mauzo yaliyosimamishwa juu ya skrini.
- Ghairi: futa mauzo haya.
Risiti
Risiti inachapishwa mara tu mauzo yakikamilika, kama mpangilio wa Chapisha ankara kiotomatiki baada ya kumaliza uko Ndiyo kwenye tawi lako (ndivyo ulivyo mwanzoni). Mtumiaji anahitaji pia ruhusa ya Chapisha Ankara; kama risiti haitoki, mmiliki aiwashe, angalia majukumu.
Kuchapisha tena risiti, gusa Miamala ya Hivi Karibuni, tafuta mauzo hayo, kisha Chapisha. Risiti hii ni risiti ya biashara: DukaPOS si EFD na haijaunganishwa na TRA.
Vitufe vilivyozimwa
Mmiliki anaweza kuficha vitufe hivi kwa jukumu fulani, au kwa kila mtu kwenye Mipangilio ya Biashara, kichupo cha POS. Kama kitufe hakionekani, wasiliana naye.
Mwisho wa zamu, funga rejista. Kwa printa, angalia printa na lebo.