Mauzo na faida
Kama una ruhusa ya faida, kitufe cha Faida ya Leo kipo juu ya kila ukurasa. Kwa uchambuzi zaidi:
- Nimepata faida kiasi gani? Fungua Ripoti ya Faida / Hasara. Chagua tawi na kipindi. Vichupo kama Faida kwa bidhaa na Faida kwa siku vinaonyesha ilikotoka faida.
- Mauzo na manunuzi yangu ni kiasi gani? Fungua Manunuzi na Mauzo. Inaonyesha Jumla ya Mauzo, Jumla ya Manunuzi, Deni la Mauzo na Deni la Manunuzi.
- Nimeuza bidhaa gani? Fungua Ripoti ya Mauzo ya Bidhaa.
- Nini kinauzika zaidi? Fungua Bidhaa Zinazopendwa.
- Malipo yaliingia kwa njia gani? Fungua Ripoti ya malipo ya mauzo. Inaonyesha pia namba za muamala.
Stoo
- Nina stoo kiasi gani? Fungua Ripoti ya Bidhaa. Chuja kwa tawi, kategoria au chapa. Inaonyesha Bidhaa Zilizopo na thamani ya Bidhaa za Kufunga.
- Nimerekebisha stoo mara ngapi? Fungua Ripoti ya Marekebisho ya Bidhaa.
- Nimenunua nini kwa msambazaji gani? Fungua Ripoti ya Manunuzi ya Bidhaa.
Fedha za kila siku
- Kila zamu ilikuwaje? Fungua Ripoti ya Rejista. Chuja kwa Mtumiaji na kipindi, angalia rejista.
- Nimetumia pesa wapi? Fungua Ripoti ya Matumizi, angalia matumizi.
- Nani ananidai na ninamdai nani? Fungua Ripoti ya Wasambazaji na Wateja, angalia madeni.
Ripoti za kufuatilia
- Ripoti ya Wakala wa Mauzo: mauzo kwa kila mfanyakazi.
- Ripoti ya Kodi: kodi iliyoandikwa kwenye mauzo na manunuzi. Ni kumbukumbu yako; DukaPOS haitumi taarifa kwa TRA.
- Kumbukumbu za Shughuli: nani alifanya nini. Inaonekana kwa akaunti ya mmiliki tu.
Ripoti zinakuwa sahihi lini?
Ripoti zinategemea kilichoandikwa. Faida inahitaji bei ya kununua kwenye kila bidhaa, manunuzi na matumizi yaliyorekodiwa. Kwa uelewa zaidi, soma jinsi ya kujua faida halisi.
Fanya ripoti kuwa tabia: angalia rejista kila siku, faida na stoo kila wiki.