Tengeneza kategoria
Fungua Matumizi > Kategoria za Matumizi, kisha ongeza kategoria zako, kwa mfano Umeme au Usafiri. Hii inakusaidia kuona pesa zinakwenda wapi. Kwenye Matumizi ya haraka unaweza pia kuongeza kategoria mpya moja kwa moja.
Ongeza matumizi moja
Kama menyu ya Matumizi haionekani, moduli imezimwa au huna ruhusa.
- 1. Fungua Matumizi > Ongeza Matumizi.
- 2. Chagua Eneo la Biashara kama una matawi zaidi ya moja.
- 3. Chagua Kategoria ya Matumizi.
- 4. Kagua Tarehe. Namba ya Kumbukumbu ukiiacha wazi, itatengenezwa yenyewe.
- 5. Kama ni mshahara wa mfanyakazi, chagua kwenye Matumizi kwa.
- 6. Andika Kiasi cha Jumla na Dokezo la matumizi.
- 7. Chini kwenye malipo, kagua Kiasi na Njia ya Malipo.
- 8. Unaweza kuambatanisha picha ya risiti kwenye Ambatisha Waraka.
- 9. Gusa Hifadhi.
Matumizi ya haraka: siku nzima kwa mara moja
Skrini hii inaonyesha kategoria zote kama POS. Inafaa kama una matumizi mengi madogo.
- 1. Fungua Matumizi > Matumizi ya haraka.
- 2. Kagua Eneo la Biashara na Tarehe.
- 3. Gusa kategoria, andika kiasi. Gusa tena kategoria hiyo kwa matumizi ya pili.
- 4. Rudia kwa matumizi mengine. Kategoria mpya inaongeza kategoria papo hapo.
- 5. Kwa siku inayofanana na iliyopita, gusa Rudia siku iliyopita na ukague kiasi.
- 6. Chagua Njia ya Malipo.
- 7. Acha alama kwenye Yamelipwa sasa, au iondoe kama bado unadaiwa.
- 8. Ukiwa na rejista iliyo wazi, acha Toa kwenye Rejista yangu ya Fedha iliyo wazi kama pesa imetoka droo.
- 9. Gusa kitufe cha kuhifadhi chini; kinaonyesha idadi ya matumizi.
Angalia matumizi
Matumizi > Orodha ya Matumizi inaonyesha yote yaliyoandikwa, kwa ruhusa yako. Kwa jumla ya kila kategoria na kipindi, fungua Ripoti > Ripoti ya Matumizi. Matumizi yanaingia pia kwenye Ripoti ya Faida / Hasara.
Muuzaji akitumia pesa za droo, zirekodi ili rejista ilingane mwisho wa zamu.