DukaPOS

Jinsi ya kutumia

Jinsi ya kuuza kwa mkopo, kupokea malipo ya deni na kutuma ukumbusho

DukaPOS inaweka deni kwa jina la mteja, kwa hiyo unaacha kutegemea kumbukumbu. Mteja lazima awe na jina kwenye mfumo.

Imesasishwa 8 Novemba 2026

Ongeza mteja na kikomo cha mkopo

  • 1. Fungua Anwani > Wateja, kisha gusa Ongeza.
  • 2. Andika Jina la Kwanza na Simu ya Mkononi. Ni lazima.
  • 3. Gusa Maelezo Zaidi kisha jaza Kikomo cha mkopo. Ukiiacha wazi, hakuna kikomo.
  • 4. Ukitaka tarehe ya kulipa, jaza Muda wa Malipo. Unaweza pia kuweka Salio la Kuanzia kama alikuwa na deni kabla.
  • 5. Hifadhi. Pia unaweza kuongeza mteja kwa kitufe cha + kwenye skrini ya POS, kama una ruhusa ya kuongeza wateja.

Uza kwa mkopo

Kitufe cha Mauzo ya Mkopo kinaonekana kama hakijazimwa kwenye Mipangilio ya Biashara, kichupo cha POS, au kwenye jukumu la muuzaji.

  • 1. Fungua skrini ya POS.
  • 2. Kwenye kisanduku cha mteja, chagua mteja halisi. Usiache Walk-In Customer, la sivyo deni halina mwenyewe.
  • 3. Weka bidhaa. Deni la Mteja linaonekana chini ya jina lake.
  • 4. Gusa Mauzo ya Mkopo.
  • 5. Kama kikomo kimepitwa, mfumo utakataa na kutaja kikomo chake.

Pokea malipo ya deni

  • 1. Fungua Anwani > Wateja. Jumla ya Deni la Mauzo inaonekana kwenye orodha.
  • 2. Gusa Vitendo kwenye mteja, kisha Lipa. Dirisha la Ongeza malipo litafunguka.
  • 3. Andika Kiasi, chagua Njia ya Malipo na Imelipwa tarehe.
  • 4. Gusa Hifadhi.
  • 5. Kwa ankara moja: Uza > Mauzo Yote, Vitendo, kisha Ongeza malipo.

Tuma ukumbusho

Kitufe hiki kinaonekana kwa akaunti ya mmiliki tu.

  • 1. Fungua Uza > Mauzo Yote, gusa Vitendo kwenye mauzo hayo, kisha Angalia Malipo.
  • 2. Kama ankara haijalipwa yote, gusa Tuma ukumbusho wa malipo.
  • 3. Kwenye dirisha, weka alama kwenye Tuma Barua pepe, Tuma SMS au Tuma arifa ya WhatsApp.
  • 4. Kagua ujumbe, kisha gusa Tuma. WhatsApp inafungua ujumbe uliotayarishwa kwenye WhatsApp yako.

Masharti ya SMS na ukumbusho wa moja kwa moja

SMS kwa wateja inahitaji akaunti yako ya SMS kwenye Mipangilio ya Biashara, kichupo cha Mipangilio ya SMS. Bila hiyo, SMS haitafika.

Unaweza kufanya ukumbusho ujitume wenyewe: Violezo vya Arifa, kichupo cha Ukumbusho wa malipo, weka alama kwenye Tuma SMS moja kwa moja au Tuma barua pepe moja kwa moja. Unatumwa kwa ankara zilizopitiliza muda wa kulipa. Kwa hiyo weka Muda wa Malipo kwa mteja.

Kwa mbinu za kudhibiti madeni, soma mwongozo wa madeni.

Maswali

Maswali ambayo wenye maduka hutuuliza

Mteja amelipa sehemu ya deni. Niweke vipi?

Fungua Vitendo > Lipa kwenye jina lake, andika kiasi alicholipa na uhifadhi. Kilichobaki kinabaki deni.

Naweza kumzuia mteja kukopa zaidi?

Ndiyo. Weka Kikomo cha mkopo kwenye taarifa zake. Mauzo ya mkopo yanayopita kikomo yanakataliwa.

Kwa nini kitufe cha ukumbusho hakionekani?

Kinaonekana kwa akaunti ya mmiliki tu, na kwa mauzo ambayo hayajalipwa yote.

DukaPOS

Fungua duka lako kwenye DukaPOS leo

Fungua akaunti, ongeza bidhaa zako na ufanye mauzo yako ya kwanza leo.